Mtine afurahia droo CAF CL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Oct 2024
Mtine afurahia droo CAF CL

Mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine amefurahia droo ya hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika Yanga ikipangwa kundi A

Yanga iko kundi A pamoja na timu za TP Mazembe, Al Hilal na MC Alger

Akizungumza baada ya droo hiyo iliyofanyika Misri jana, Mtine alisema Yanga ilipata kile ilichohitaji katika hatua ya makundi

"Nafuraha kwa sababu tumepata kile tulichohitaji. Nafikiri tuna nafasi ya kufanya vizuri katika kundi hili"

"Yanga tuna timu nzuri sana naamini tutakuwa na wakati mzuri katika michuano hii msimu huu," alisema Mtine

Akiizungumzia mechi mbili dhidi ya TP Mazembe ambazo Yanga watakabiliana nazo hatua ya makundi, Mtine alisema malengo ni kupata alama sita dhidi ya yao

"TP Mazembe ni familia yangu, lakini kwa sasa niko Yanga tunataka kuwafinga hapa nyumbani na kwao pia," aliongeza Mtine ambaye alifanya kazi na TP Mazembe kwa takribani miaka 12 kabla ya kutua Yanga

Mtine ameongeza kuwa msimu Yanga imeweka malengo makubwa katika michuano ya ligi ya mabingwa lakini kila jambo litafanyika hatua kwa hatua

"Kwanza tunahitaji kuhakikisha tunaingia robo fainali, baada ya hapo tutaweka mkakati mwingine wa kwenda nusu fainali na hatua nyingine zitakazofata," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’