Yanga imeondoka na alama zote tatu uwanja wa Azam Complex baada ya kuichapa KMC bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Bao pekee la Yanga lilifungwa na Maxi Nzengeli katika dakika ya tano akimalizia shambulizi la mapema lililofanywa na Yanga
Pengine unaweza kusema Wananchi walikosa bahati leo kwani walifanya mashambulizi mengi katika lango la KMC lakini kilichokosekana ni mpira kuingia nyavuni kuiandikia Yanga mabao zaidi
Ni ushindi muhimu ambao unaisogeza Yanga hadi nafasi ya nne katika msimamo wa ligi huku ikiwa na mechi tatu za viporo
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Fiston Mayele leo alikuwa jukwaani sambamba na Rais Injinia Hersi Said wakishuhudia mchezo huo
ADVERTISE HERE