Yanga imefanikiwa kuondoka na alama zote tatu mkoani Mbeya wakiichapa Ken Gold bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sokoine
Bao pekee la Yanga lilifungwa na beki Ibrahim Bacca dakika ya 13 akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Aziz Ki
Unaweza kusema mpango wa kujihami uliotumiwa na Ken Gold uliibeba timu hiyo katika mchezo huo wakijilinda zaidi na kushambulia kwa kushitukiza
Mlinda lango wa Ken Gold pia alifanya kazi nzuri kuokoa michomo kadhaa iliyopelekwa langoni kwake hasa katika kipindi cha pili huku Djigui Diarra nae akifanya kazi nzuri dakika za majeruhi kuhakikisha Yanga inaondoka na alama tatu muhimu
Ni ushindi wa pili mfululizo kwa Yanga ugenini, alama sita na mabao matatu
ADVERTISE HERE