Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto sio miongoni mwa wachezaji walioko Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili kuwania kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CBE SA
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa Mwamnyeto alipewa ruhusa kurejea jijini Dar es salaam ili kushughulikia matatizo ya kifamilia
Kamwe amesema Shekhan Khamis na Farid Mussa ambaye ni majeruhi pia wataukosa mchezo huo. Shekhan yuko katika kikosi cha timu ya Taifa ya vijana U20
Wachezaji wengine wote wako tayari kwa mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 2:30 usiku Yanga ikihitaji ushindi au sare ili kutinga hatua ya makundi CAF CL
ADVERTISE HERE