Hivi ndivyo Yanga itafyeka kichaka cha CAF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Sep 2024
Hivi ndivyo Yanga itafyeka kichaka cha CAF

Ukiangalia 'ranking' za CAF kwa msimu huu 2024/25 Yanga inashika nafasi ya 13 ikiwa na alama 31 huku watani zao Simba wakiwa nafasi ya 7 wakiwa alama 39

Msimamo huo ukichukuliwa kwa msimu ujao yaani 2025/26 pasipo kujali matokeo ya msimu huu, Yanga itabaki na alama 24 na kusogea nafasi ya 12 huku watani zao Simba wakibaki na alama 28 na kusogea mpaka nafasi ya 6

Kama Yanga haitafuzu hatua ya makundi CAF CL itapoteza alama 7 wakati kama Simba watashindwa kufuzu hatua ya makundi CAF CC watapoteza alama 11

Lakini kama Yanga itaifunga CBE na kufuzu hatua ya makundi CAF CL wataongeza alama 5 na kufikisha alama 29 wakati watani zao Simba wakifuzu hatua ya makundi CAF CC wataongeza alama 2.5 na kufikisha alama 30.5

Yaani hadi kufikia Jumatatu pengine tofauti ya alama katika ranking za CAF kati ya Yanga na Simba inaweza kuwa 1.5 tu kama timu zote zitafuzu hatua ya makundi

Kama itatokea Yanga ikafuzu makundi halafu watani zao Simba wakashindwa kufuzu,Β  itakuwa rasmi Yanga 'imefyeka kichaka' cha ranking za CAF!

Vyovyote itakavyokuwa msimu huu Yanga ina nafasi nzuri zaidi ya kukaa juu ya Simba katika ranking za CAF, kinachohitajika ni angalau kufika robo fainali kama msimu uliopita

Kama Yanga itafika robo fainali CAF CL, Simba watahitaji kufika nusu fainali CAF CC ili kupata alama sawa na Yanga

Ikitokea Wananchi wakavuka hadi nusu fainali basi Simba watahitaji kuwa mabingwa wa CAF CC ili kupata alama sawa na Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’