FT : Mbeya City 1-1 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Apr 2018
FT : Mbeya City 1-1 Yanga
Yanga imeshindwa kupunguza tofauti ya pointi baina yake na vinara wa ligi Simba baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbeya City kwenye mchezo wa ligi hiyo uliopigwa kwenye dimba la Sokoine.

Yanga ilitangulia kupata bao la kuongoza kwenye dakika ya 57 mfungaji akiwa Raphael Daudi Lothi aliyeunganisha vyema mpira wa adhabu uliopigwa na Juma Abdul.

Licha ya kuwa pungufu baada ya nahodha wao Ramadhani Malima kupewa kadi ya pili ya njano baada ya kumwangusha Yusuph Mhilu kwenye dakika ya 65, Mbeya City ilifanikiwa kusawazisha kwenye dakika ya 90 kupitia kwa mpira wa kichwa wa Iddy Naddo.

Mchezo huo uligubikwa na vurugu za mara kwa mara kutoka kwa mashabiki wa Mbeya City muda mfupi baada ya timu yao kufungwa.

Mashabiki hao walimrushia mawe na chupa mlinda lango wa Yanga Youthe Rostand aliyelazimika kukimbia langoni.

Jeshi la Polisi lililazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki wa Mbeya City waliokuwa wakifanya vurugu.

Mchezo huo uliendelea baada ya vurugu hizo kutulia.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’