Gamondi apania kuweka rekodi Ethiopia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Sep 2024
Gamondi apania kuweka rekodi Ethiopia

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ameweka bayana kuwa kikosi chake kinakwenda Ethiopia wakiwa na dhamira moja tu, kuhakikisha wanashinda ugenini ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika kwa msimu wa pili mfululizo

Yanga itacheza mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya CBE SA Jumamosi Septemba 14 na timu hizo kurudiana wiki moja baadae nchini Tanzania

Msafara wa Yanga utaondoka nchini Alfajiri ya kesho Alhamisi ambapo utajumuisha baadhi ya wachezaji huku miongoni mwa wachezaji waliokuwa katika majukumu ya timu za Taifa wakitarajiwa kujiunga na timu moja kwa moja Ethiopia

Historia inaonyesha Yanga imekuwa na wakati mgumu kupata ushindi katika ardhi ya Ethiopia ambapo mara ya mwisho Wananchi kucheza nchini humo, walichapwa bao 1-0 na Wolaita Ditcha ukiwa mchezo wa raundi ya kwanza kombe la Shirikisho (CAF CC)

Hata hivyo wakati huu Yanga inajivunia kuwa na kikosi bora lakini Gamondi amesema hilo halitoshi, ni lazima wakapambane kusaka ushindi ugenini

Gamondi amesema amewafuatilia CBE na kubaini ubora na udhaifu wao na hivyo anafahamu aina ya mchezo wanaokwenda kukabiliana nao

"Nimeangalia timu yao ina wachezaji wachache ambao wamejiunga na timu ya Taifa ya Ethiopia tofauti na sisi ambapo tuna wachezaji kama 14 wanaoyatumikia mataifa yao"

"Hatua hiyo inaifanya timu yao nzima kubaki ikijiandaa vizuri kulinganisha na sisi, lakini hilo sio tatizo, tuna kikosi imara kitakachoweza kufanya vizuri endapo tu wachezaji wangu wote watarejea kwa wakati na wakiwa fiti"

"Tunakwenda Ethiopia tukiwa tunafahamu kwamba tunahitaji kupata matokeo mazuri ambayo yatatupa nguvu zaidi tutakaporudiana nyumbani. Tunataka kuona tunashinda kwao na kwetu," alisema Gamondi

CBE SA ndio mabingwa wa ligi kuu ya Ethiopia ambapo walifanikiwa kuvuka hatua ya awali kwa kuichapa SC Villa ya Uganda kwa mabao 3-2. Walishinda 2-1 ugenini na kulazimishwa sare ya bao 1-1 nyumbani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’