Dharau itawaponza Simba kwa Kagoma

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Sep 2024
Dharau itawaponza Simba kwa Kagoma

Ukweli ni kuwa Yanga haikuwa na ulazima wa kufufua sakata la usajili wa mchezaji Yusuph Kagoma ambaye alisaini Simba wakati akiwa pia amesaini mkataba halali wa kuitumikia Yanga

Lakini dharau, kejeli na kashfa kutoka Simba ni kama zimepelekea Yanga kumuwekea pingamizi mchezaji huyo

Yanga ilikamilisha usajili wa Kagoma muda mrefu, mwishoni mwa mwezi March 2024 ambapo ilimalizana na Singida FG kwa ajili ya kuwasajili pamoja na Nickson Kibabage

Kagoma alisaini mkataba halali wa kuitumikia Yanga ambapo makubaliano ya kimkataba ilikuwa malipo yake kukamilishwa Julai 01, Yanga walikamilisha kama mkataba ulivyoelekeza

Kilichotokea baada ya msimu kumalizika Kagoma akashawishiwa na watu wa upande wa pili ambao walimuhakikishia kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza hasa ikizingatiwa walikuwa wanaunda timu mpya

Bila ya kuzingatia makubaliano yake na Yanga, Kagoma akakubali kusaini Simba, huku viongozi wa timu hiyo hasa msemaji wao wakitoa kejeli kwa Yanga

Yanga ilimpa Kagoma nafasi ya kukiri kufanya kosa na kuomba radhi hadharani ili asamehewe aitumikie timu yake hiyo mpya

Lakini pia atalazimika kulipa fidia ya gharama ambazo Yanga ilitumia wakati inamsajili. Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya TFF imemsimamisha mchezaji huyo hadi pale shauri lake litakapomalizika

Kagoma tayari ameitumikia Simba katika mechi mbili za ligi kuu hivyo kama itathibitishwa ni mchezaji halali wa Yanga maana yake ni kuwa Simba walimtumia mchezaji ambaye sio wao na hivyo wanapaswa kupoteza mechi zote mbili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’