Saa 10 jioni leo kupitia Yanga App, Mwananchi utapata fursa ya kushuhudia dakika 90 za mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Kiluvya Fc uliopigwa uwanja wa KMC Complex mapema leo
Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, Jean Baleke akifunga moja ya mabao hayo
Salum Abubakar 'Sure Boy' na Shekhan Ibrahim nao walizifumania nyavu katika mchezo huo ambao kocha Miguel Gamondi alitumia nyota wake waliobaki ambao hawakuwa na majukumu ya timu za Taifa
Yanga inaendelea na maandalizi ya mechi mbili za kuwania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa dhidi ya CBE SA ya Ethiopia
ADVERTISE HERE