New Amaan Complex yaandaliwa kuipokea Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Sep 2024
New Amaan Complex yaandaliwa kuipokea Yanga

Wiki iliyopita, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alidokeza dhamira ya mabingwa hao wa Tanzania Bara kwa misimu mitatu mfululizo kupeleka visiwani Zanzibar mechi ya marudiano ya raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa dhidi ya CBE SA ya Ethiopia. Yanga itaanza ugenini na kumalizia nyumbani

Taarifa kutoka ndani ya Shirikisho la soka Zanzbar (ZFF), imethibitisha kuwa maandalizi yameanza baada ya kupata uthibitisho kutoka Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) ambalo limewataarifu juu ya mchezo huo kupigwa Zanzibar

Katibu Mkuu wa ZFF, Hussein Ahmada amesema tayari ZFF na wadau wake wameshaanza maandalizi ya kuupokea mchezo huo ambao utatoa hatma ya Yanga katika kusaka rekodi ya kucheza makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya pili mfululizo.

"Ni kweli CAF wameshatujulisha kwamba huu mchezo utatumika kwenye uwanja wetu wa New Amaan kama ambavyo timu mwenyeji wa mchezo huo Yanga walivyoomba"

"Sisi kama ZFF kwanza tunawashukuru Yanga kwa uamuzi huo wa kizalendo, Zanzibar ni sehemu ambayo ina mashabiki wengi lakini pia hata wale ambao watatoka bara hapa ni rahisi kufika"

"Hivyo sisi kama ZFF tumeshaanza maandalizi kwa haraka, kujiandaa na kupokea wageni kwa timu zote lakini pia mashabiki wao tunaamini Uwanja wa Amaan utakuwa ni baraka kwa Yanga kushinda kwa kishindo na hata kufuzu kuingia makundi na pengine kwenda mbali zaidi," Ahmada alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

Hii itakuwa mara ya pili Yanga kucheza mech kubwa ya mashindano katika uwanja wa New Amaan Complex baada ya kufanyiwa maboresho

Yanga ilikamilisha msimu uliopita kwa kutwaa kombe la Shirikisho la CRDB katika uwanja huo kwa kuifunga Azam Fc mikwaju ya penati 6-5 baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’