Mshambuliaji Jean Baleke bado anapambana kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Yanga
Mara ya mwisho Baleke kuonekana dimbani ni katika mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Red Arrows akitumika dakika 45 za kipindi cha kwanza
Mcongomani huyo hakutumika katika mechi za awali ligi ya mabingwa dhidi ya Vital'o kama ilivyo kwa Chadrack Boka baada ya ITC zao kuchelewa. Hata hivyo wote wanaweza kutumika katika mechi inayofuata dhidi ya CBE SA
Alikosa mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambapo pia hakuwa miongoni mwa wachezaji 20 waliosafiri Kagera
Lakini bila shaka Baleke ataonekana katika mechi zijazo na pengine mechi dhidi ya CBE anaweza kutumika
Beleke ni mshambuliaji pekee aliyebaki kikosini baada ya Clement Mzize, Prince Dube na Kennedy Musonda kuitwa timu za Taifa
Msimu huu eneo la ushambuliaji ushindani ni mkali, Dube na Mzize wameanza vyema na kujihakikishia nafasi zaidi katika kikosi cha Gamondi