Yanga imeanza vyema msimu wa ligi kuu ya NBC 2024/25 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliopigwa uwanja wa Kaitaba
Alikuwa ni Maxi Nzengeli aliyefungua ukurasa wa mabao kwa Yanga msimu huu akifunga bao la uongozi kwenye dakika ya 26 kwa shuti la nje ya 18
Pengine Yanga ingefunga mabao zaidi katika kipindi cha kwanza kama sio uimara wa mlinda lango Ramadhan Charamanda aliyeokoa michomo hatari ya Prince Dube ambaye pia atajilaumu kwa kushindwa kutumia nafasi adimu
Kipindi cha pili Yanga ilipunguza kasi na kuwapa wenyeji Kagera Sugar kutawala mchezo hata hivyo alikuwa ni Clement Mzize 'super sub' aliyefunga bao la pili dakika ya 89 akimalizia pasi murua kutoka kwa Stephane Aziz Ki
Ni alama tatu muhimu kibindoni kwa Yanga wakizipata katika moja ya viwanja vigumu kuondoka na alama tatu