Yanga yapiga hesabu za kutinga robo fainali CAF CC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Apr 2018
Yanga yapiga hesabu za kutinga robo fainali CAF CC
Wakati droo ya Makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika ikitarajiwa kufanyika leo jiji la Cairo nchini Misri, klabu ya Yanga inajipanga kufanya vizuri katika michuano hiyo mwaka huu.

Mwaka 2016 Yanga ilitinga hatua ya makundi lakini ilishindwa kufanya vizuri ikimaliza nafasi nne kwenye kundi A baada ya kujikusanyia alama nne.

Mwaka 2016 Yanga ilipangwa kundi A sambamba na TP Mazembe(DRC), Medeama(Ghana) na MO Bejaia(Algeria)

Nahodha wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema mwaka huu wamejipanga kuhakikisha wanavuka hatua hiyo ya makundi.

Timu mbili za juu kutoka kila kundi zitatinga robo fainali ya michuano hiyo na kujinyakulia kitita cha zaidi ya Tsh Milioni 800.

Ò€œMwaka 2016 tulifanikiwa kufikia mafanikio haya ya kutinga hatua ya makundi lakini hatukuvuka hapo, safari hii lazima tujipange na kuhakikisha tunajiandaa vyema ili kuvuka hatua hii, hayo yatakuwa mafanikio kwetu,Ò€ alisema Cannavaro baada ya Yanga kuwasili kutoka Ethiopia.

Yanga inatarajiwa kuondoka leo mchana kwa usafiri wa Ndege kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mbeya City
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’