Wakongwe washauri Yanga iimarishe kiungo, ushambuliaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Apr 2018
Wakongwe washauri Yanga iimarishe kiungo, ushambuliaji
Mdau wa klabu ya Yanga Mohammed Kampira pamoja na beki wa zamani wa timu hiyo Keneth Pius Mkapa wamesema Yanga inahitaji kujiimarisha zaidi kwenye nafasi kiungo na ushambuliaji ili ifanye vizuri kwenye michuano ya kombe la Shirikisho hatua ya makundi.



Pichani Kenneth Mkapa enzi zake akiwa na Marehemu Said Mwamba, mwaka 1993

Yanga imetinga hatua ya makundi baada ya kuiondoa Wolaitta Dicha kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1 licha ya kufungwa bao 1-0 nchini Ethiopia juzi.

Akizungumza katika kipindi cha Yanga TV, Mkapa amesema hana mashaka na safu ya ulinzi ya Yanga lakini ni dhahiri kunahitajika uwekezaji zaidi katika nafasi ya kiungo na ushambuliaji.

Amesema katika mchezo dhidi ya Dicha Yanga ilikosa muunganiko mzuri kutoka kwenye kiungo na ushambuliaji.

Amesema si vibaya kama Yanga itasajili kiungo mwenye uwezo zaidi wa kulisha mipira kwa washambuliaji.

Naye Kampira amemkosoa kiungo Pius Buswita na kumtaka abadili aina yake ya uchezaji ili aweze kuisaidia zaidi timu.

"Katika mchezo dhidi ya Dicha, kuna wakati Chirwa alikuwa peke yake mbele akikabwa na watu wanne, Buswita alitakiwa kusaidiana nae"

"Buswita ni mchezaji mzuri lakini inabidi aache utoto ili aweze kudhihirisha ubora wake"

Kuelekea hatua ya makundi Yanga ina nafasi ya kusajili mchezaji/wachezaji kukamilisha idadi ya wachezaji 30 kama orodha ya awali iliyotumwa CAF mwezi Januari ni pungufu ya wachezaji hao.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’