Gamondi azidi kumuongeza makali Dube

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Aug 2024
Gamondi azidi kumuongeza makali Dube

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi anaamini mshambuliaji Prince Dube atafunga mabao mengi msimu huu kama atazingatia maelekezo anayopatiwa katika kiwanja cha mazoezi

Dube ameanza vyema maisha yake na Yanga akipachika mabao manne, assist mbili katika mechi saba alizowatumikia Wananchi mpaka sasa

Gamondi amesema Dube ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa akiwa na wastani mzuri wa kupiga mashuti yanayolenga lango

Amesema kuna maelekezo ameendelea kumpatia ili kumfanya awe bora zaidi

"Nimemwambia azingatie mambo mawili. La kwanza kucheza zaidi ndani ya boksi la wapinzani, pili atulize presha, asiwe na haraka katika kuzitumia nafasi ambazo timu inazitengeneza, akifanya hivyo ataweza kuongeza idadi ya mabao kwa kuwa timu ina uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi"

"Dube ni mshambuliaji bora mwenye akili nyingi, nguvu na kasi lakini zaidi uwezo wa kulenga (target) ambavyo sio rahisi kwa mshambuliaji kupata vyote hivyo, wengi unaweza kuwakuta wana sifa moja au mbili tu," alisema Gamondi

Dube alitua Yanga katika dirisha lililopita akitokea klabu ya Azam Fc aliyoachana nayo mwezi Machi mwaka huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
16m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’