Kuna uwezekano mkubwa Yanga itachuana na CBE ya Ethiopia katika mchezo wa kusaka tiketi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kama timu hiyo italinda ushindi wa ugenini iliyopata dhidi ya SC Villa ya Uganda katika mchezo wa mkondo wa kwanza
CBE ndio mabingwa wa ligi kuu ya Ethiopia wakitwaa ubingwa huo msimu uliopita ikiwa ni mara yao ya kwanza na kukata tiketi ya michuano ya ligi ya mabingwa. Waliichapa SC Villa mabao 2-1 nchini Uganda
Aidha kwa upande wa Yanga, baada ya ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Azam Complex Jumamosi iliyopita, Kocha Miguel Gamondi aliwapa wachezaji wake mapumziko ya siku moja
Akizungumza baada ya mchezo huo, Gamondi alisema licha ya ushindi huo mnono, bado kikosi chake hakijafuzu hatua inayofuata hadi pale watakapowatoa Vital'o
"Bado hatujafuzu, hizi ni dakika 90 za kwanza nani anajua kipi kitatokea katika mchezo wa marudiano, tutapumzika kwa siku moja baada ya hapo tutarudi kujipanga kwa mechi hiyo," alisema Gamondi
Katika mchezo wa marudiano Yanga inahitaji ushindi au sare tu ili kusonga mbele hatua inayofuata na kama SC Villa watashindwa kupindua matokeo ugenini wakihitaji kushinda kuanzia mabao 2-0, wataipa nafasi Commercial Bank ya Ethiopia kusonga mbele na kuchuana na Yanga
Habari njema kwa Yanga ni kuwa changamoto ambazo CBE wamekutana nazo hazina tofauti na changamoto walizokutana nazo Vital'o, kwani timu hizo hazichezi mechi zao za nyumbani katika nchi zao kwa kuwa hawana viwanja vinavyokidhi vigezo vya CAF