Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amewapongeza wachezaji wake baada ya kutwaa Ngao ya Jamii kufuatia ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Azam Fc katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jana
Yanga ilitokea nyuma katika mchezo huo Azam Fc wakifunga bao la mapema dakika ya 13 kupitia kwa Feisal Salum ambaye aina yake ya ushangiliaji ni kama iliamsha 'majini' ya Wananchi
Iliwachukua Yanga dakika tano tu kurejesha bao hilo kupitia kwa Prince Dube kabla ya Boka kusababisha la pili ambalo Azam walijifunga na kisha Aziz Ki na Clement Mzize kuongeza mabao mengine mawili
Akizungumza baada ya mchezo huo Gamondi alisema vijana wake walionyesha ukomavu wa hali ya juu
"Nawapongeza wachezaji wangu wameonyesha kiwango bora kwani licha ya kuruhusu bao mapema, hawakutoka mchezoni na hatimaye kusawazisha na kufunga mabao mengine matatu"
"Mara nyingi nimekuwa nikiwaambia wachezaji wangu tunapaswa kucheza kama tunafanya mazoezi, leo tumefanya hivyo, tulikuwa bora na tumestahili kushinda Ngao hii ya jamii"
"Tumekuwa na maandalizi mazuri ya msimu tangu tulipoweka kambi Afrika Kusini, ni mwanzo mzuri kwetu kuwafunga wapinzani wetu Simba na Azam Fc katika michuano hii," alisema Gamondi
Kituo kinachofauta kwa Yanga sasa ni mechi ya hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Vital'o ambapo mechi ya mkondo wa kwanza itapigwa Jumamosi August 17 katika uwanja wa Azam Complex