Mchambuzi na Mwanahabari mkongwe Edo Kumwembe amemshukia Elly Sasii, mwamuzi wa mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga dhidi ya Simba uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jana
Katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kutinga fainali ya michuano hiyo, Sasii alishindwa kuumudu akiinyima Yanga bao halali lililofungwa na Stephane Aziz Ki katika kipindi cha pili huku pia akigoma kutoa penati kwa timu zote mbili katika matukio tofauti
Aidha pia kulikuwa matukio mengi ya faulo yalichukuliwa hatua upande wa Yanga lakini matukio kama hayo hayakuchukuliwa hatua upande wa Simba
"Ahmed Arajiga anaendelea kuwa mwamuzi bora nchini. Angekuwa uwanjani angewapa Yanga penalti na angewapa Simba penalti"
"Arajiga ana guts za maamuzi magumu mechi hizi. Huyo dogo aliyepewa mechi aliniblock zamani insta kwa sababu mara nyingi nilikuwa namfuata DM kumwambia ukweli kuwa anaharibu mechi. Hata hivyo hauhusiki katika bao la Aziz Ki, sio kazi yake. Ni ya msaidizi wake," sehemu ya maoni ya Kumwembe aliyotoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Hii sio mara ya kwanza kwa Sasii kuingia lawamani pale anapochezesha mechi zinazohusisha klabu ya Yanga
Utaona ni kwa nini baada ya TFF kumtangaza Sasii kuchezesha mechi hiyo ya dabi, mashabiki wengi wa Yanga walitoa maoni tofauti