Kwa Yanga hii wachague wenyewe kikosi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Aug 2024
Kwa Yanga hii wachague wenyewe kikosi

Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga wako katika nyakati nzuri sana kutokana na ubora wa kikosi chao

Aidha maboresho ya usajili ambayo yamefanyika katika dirisha hili ni kama kuongeza kachumbari katika chakula ambacho kilikuwa tayari

Wakati Yanga leo ikishuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakabili watani zao Simba, Wananchi wanakwenda kifua mbele wakiwa na timu bora zaidi

Pengine hii ndio sababu inayowafanya mashabiki wa Yanga wasiwe na hofu kuelekea mchezo huo kulinganisha na watani zao Simba ambao hawana uhakika na timu yao ambayo ina kundi kubwa la wachezaji wageni

Ukiangalia vikosi viwili ambavyo Gamondi alivitumia katika mchezo dhidi ya Red Arrows, chochote anaweza kukitumia leo na wananchi wakaondoka na furaha dimba la Mkapa

Yaani Gamondi anaweza kuwapa nafasi wapinzani wake wachague timu ya kukabiliana nayo na mambo bado yanaweza yakawa magumu upande wao

Lakini hii ni mechi ambayo Gamondi na vijana wake waliisubiri sana kwa hamu. Msimu uliopita Yanga ilikosa Ngao ya Jamii na kupoteza nafasi ya kushinda 'treble'

Yanga ilipoteza mchezo dhidi ya Simba kwa mikwaju ya penati baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana mkoani Tanga

Hivyo hii ni kama mechi ya kisasi kwa Yanga, Gamondi hayuko tayari kuona timu yake inapoteza mechi dhidi ya Simba kwenye Ngao ya Jamii kwa mara nyingine

Jana katika Mkutano na waandishi wa habari, Gamondi aliweka wazi umuhimu wa mchezo wa leo, alisema anaheshimu mechi za dabi na hivyo watakwenda kucheza mechi hii wakiwa na kikosi chao bora zaidi pamoja na kuchukua tahadhari zote ili kuhakikisha wanashinda

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’