Jana Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Red Arrows katika mchezo wa kuhitimisha wiki ya Mwananchi uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa mbele ya mashabiki 60,000
Mabao yote mawili ya Yanga yalipatikana katika kipindi cha pili kupitia kwa Mudathir Yahya na Stephane Aziz Ki (p) ambao wote waliingia katika kipindi hicho
Alichofanya kocha wa Yanga Miguel Gamondi katika mchezo huo ni kuficha mbinu na silaha zake ambazo atazitumia August 08 katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba
Alitumia wachezaji 24 katika mchezo huo ambapo kila kipindi alitumia kikosi tofauti huku baadhi ya wachezaji akiwatumia katika maeneo ambayo hayajazoeleka
Mfano Denis Nkane aliyeingia kipindi cha pili alitumika kama mlinzi wa kulia na baadae majukumu hayo akayafanya Maxi Nzengeli
Aziz Andambwile alitumika kama mlinzi wa kati katika kipindi cha kwanza akianza na Dickson Job kabla ya Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca kuingia kuchukua nafasi zao katika kipindi cha pili
Kama kocha wa Simba alipanga kutumia mchezo huo kubaini mbinu na kikosi ambacho Gamondi atakitumia August 08 basi ni wazi ametoka patupu
Hakuna mchezaji aliyecheza zaidi ya dakika 45 upande wa Yanga, hivyo si rahisi kubaini kikosi kilichoandaliwa kwa ajili ya August 08 ni kipi