Hatimaye August 04 imefika! Ni siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki na wanachama wa Yanga ambapo utambulisho rasmi wa kikosi kwa ajili ya msimu huu utafanyika
Wananchi wanasema tukio lililofanyika jana uwanja wa Benjamin Mkapa ulikuwa utangulizi, shughuli rasmi ni leo
Takribani mashabiki 60,000 wataujaza uwanja wa Benjamin Mkapa mbapo mageti yanatarajiwa kufunguliwa mapema tu, saa 5 asubuhi
Burudani itaanza na mechi za utangulizi ambazo zitahusisha Yanga U20, Yanga Princess, Yanga malegendary, Wafanyakazi wa Yanga dhidi ya wasanii
Lakini pia Harmonize ataongoza kundi la wasanii mashuhuri nchini kuwapa burudani Wananchi
Tukio la utambulisho wa kikosi litafuata baada ya mfululizo wa burudani ambapo Dakota, Maulid Kitenge na Haji Manara wataifanya kazi hiyo
Mchezo wa kuhitimisha siku ya Wananchi leo ni kati ya Yanga dhidi ya Red Arrows mabingwa ligi kuu ya Zambia na kombe la Kagame na utapigwa majira ya saa 1 usiku