Yanga yaweka rekodi mauzo ya jezi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jul 2024
Yanga yaweka rekodi mauzo ya jezi

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Haji Manara leo amefichua kuwa ndani ya siku tatu tangu ilipozindua jezi, nakala zaidi ya laki tano zimeuzwa

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo ambao waliufanya pamoja na Meneja wa Habari na Mawasiliano Ali Kamwe, Buggati aliwataka mashabiki wa Yanga kutembelea madukani kununua jezi zao ili kuhakikisha kila mmoja anakwenda kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi siku ya Jumapili akiwa na jezi mpya

"Nimearifiwa tayari tumemaliza mzigo wote, kwa wasiofahamu tumeuza nakala zaidi ya laki tano za jezi. Hivyo kila Mwananchi ahakikishe anatembelea duka letu pale Makao Makuu ya klabu au Mawakala wetu kujipatia jezi yake"

"Tuhakikishe katika kilele cha Wiki ya Mwananchi kila mmoja anakuja akiwa amependeza na jezi mpya," alisema Manara

Yanga imefunga mauzo ya jezi za jumla na kuwataka wafanyabiashara kufika Makao Makuu ya Yanga kununua jezi zao kwa bei ya rejareja ambayo ni Tsh 45,000/-

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’