Tunaanza na Wiki ya Wananchi wa Kaizer Chiefs

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jul 2024
Tunaanza na Wiki ya Wananchi wa Kaizer Chiefs

Fainali ya Toyota Cup inapigwa leo huko Afrika Kusini ambapo mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga watakuwa wageni wa Kaizer Chiefs

Ni mchezo maalum kwa Kaizer Chiefs kukaribisha msimu mpya wa mashindano yaani ni kama kilele cha Wiki ya Mwananchi

Msimu uliopita Kaizer Chiefs walialikwa na Yanga katika tukio kama hilo mchezo ukipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Kennedy Musonda akifunga bao pekee la ushindi wa Yanga baada ya pasi ya Maxi Nzengeli

Chiefs wakavutiwa na tamasha hilo na hivyo nao kuandaa mwaka huu huku wadhamini wao Toyota wakinogesha kwa kuweka zawadi na kombe kwa timu itakayoshinda mchezo huo

Kwa Yanga huu ni mchezo muhimu ukiwa ni mwendelezo ya maandalizi kuelekea msimu ujao 2024/25 huo ukiwa mchezo wa tatu Yanga inacheza

Ni mechi inayotarajiwa kuwa na ushindani kwani inakutanisha makocha wawili 'wa Yanga'

Nasreddine Nabi alikuwaa kocha wa Yanga kabla ya kutimikia Morocco na msimu huu kujiunga na Kaizer Chiefs

Gamondi alitua Yanga baada ya Nabi kuondoka msimu uliopita, leo atataka kudhihirisha ubora wake mbele ya Nabi ambaye bado heshima yake inaishi Jangwani

Mchezo utapigwa saa 10 jioni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’