Kila mchezaji atapata nafasi pre-season - Walter

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jul 2024
Kila mchezaji atapata nafasi pre-season - Walter

Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema kila mchezaji ambaye yupo kwenye kikosi cha Yanga kinachoendelea na maandalizi ya msimu mpya, atapata nafasi ya kucheza katika mechi wanazocheza huko Afrika Kusini

Jana Yanga ilifanya mazoezi maalum ya 'recovery' baada ya mchezo dhidi ya Ausburg ambapo Jumatano, Julai 24 Yanga itacheza mechi ya pili dhidi ya TS Galaxy

Walter amesema wanatarajia katika mchezo huo watawatumia wachezaji ambao hawakucheza mechi iliyopita dhidi ya Ausburg

"Leo (jana) tumefanya mazoezi ya aina tofauti kwa wachezaji waliocheza mechi dhidi ya Ausburg na wale ambao hawakucheza kabisa"

"Tunatafuta uwiano kuona vile tunaweza kuwatumia wachezaji ambao hawakupata nafasi katika mchezo uliopita lengo ni kuwa na usawa wa dakika ambazo kila mmoja ambaye tumekuja nae hapa anacheza," alisema Walter

Mchezo dhidi ya TS Galaxy hautaonyeshwa 'mbashara' na pia hautakuwa na mashabiki lakini Wananchi wataonekana tena 'live' Julai 28 katika mchezo wa Toyota Cup dhidi ya Kaizer Chiefs

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’