Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amesisitiza hajamaliza kazi iliyomleta Tanzania katika klabu ya Yanga na ndio sababu ameendelea kusalia na mabingwa hao wa nchi
Jana baada ya mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Mpumalanga International Cup dhidi ya Augsburg uliomalizika kwa Yanga kupoteza kwa mabao 2-1, wanahabari walifanya mahojiano na Aziz Ki wengi wakitaka kufahamu imekuwaje ameendelea kubaki Yanga baada ya kiwango kikubwa alichoonyesha msimu uliopita
Aidha wengine walitaka kufahamu kama alipokea ofa yoyote kutoka timu za hapo Afrika Kusini
"Nilipokea ofa hapa Afrika Kusini lakini kwangu ilikuwa rahisi kubaki Yanga kwa sababu bado kuna kazi sijaimaliza hapa"
"Nataka kuona Yanga kuwa miongoni mwa timu kubwa barani Afrika lengo letu msimu huu ni kucheza nusu fainali na hata fainali ya ligi ya mabingwa"
"Nafurahi timu imeongeza wachezaji bora na wazoefu zaidi, naamini tutakuwa bora pengine kuliko msimu uliopita," alisema Aziz Ki
Aidha Ki amewataja Clatous Chama, Jean Baleke, Prince Dube na wachezaji wengine waliosajiliwa uzoefu wao utasaidia kufikia malengo ya klabu msimu huu
"Nafurahi kucheza na Chama timu moja, yeye ni mchezaji mwenye uzoefu kuliko mimi lakini pia ujio wa akina Dube, Baleke na wengine nadhani utatufanya tuwe bora zaidi"