Kiungo wa Yanga Khalid Aucho tayari amerejea nchini kuungana na wenzake ambao walianza pre-season mwanzoni mwa wiki hii
Wachezaji waliokuwa na majukumu ya timu za Taifa walipewa siku zaidi za mapumziko licha ya kuwa baadhi walirejea mapema
Aucho, mlinda lango Djigui Diarra, Kennedy Musonda, Stephane Aziz Ki, Bakari Nondo Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Mzize, Mshery na Mudathir ni baadhi ya wachezaji ambao walikuwa na majukumu ya timu za Taifa baada ya msimu kumalizika na hivyo kupewa muda zaidi wa kupumzika
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi leo alitoa mapumziko kwa wachezaji wote, watarejea Avic Town Jumatatu kuendele na maandalizi
Kuanzia Jumatatu wachezaji wote wanatarajiwa kuwa Avic Town
ADVERTISE HERE