Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema watahitaji kuwa bora zaidi msimu huu ili kuweza kutetea mataji waliyoshinda msimu uliopita pamoja na kufanya vizuri zaidi katika ligi ya mabingwa barani Afrika
Kutokana na usajili ambao Yanga wamefanya katika dirisha hili, Wananchi wana matumaini makubwa kuendelea kugawa dozi katika ligi kuu ya NBC na kufika mbali zaidi kwenye ligi ya mabingwa
Gamondi amesema wameanza maandalizi mapema kwa kuwa wanafahamu ili kufikia malengo na matarajio hayo inawapasa kuwa bora zaidi
"Haitakuwa rahisi ni lazima tuimarike na kuwa bora zaidi ya tulivyokuwa msimu uliopita. Nafahamu kila timu inajiandaa kwa ajili ya kukabiliana na Yanga hivyo pamoja na usajili mzuri tuliofanya, tunapaswa kuongeza ubora wetu uwanjani"
"Kama klabu, msimu huu tunataka kuweka alama katika soka la Afrika, tunataka kuona Yanga inakuwa mongoni mwa timu tano bora barani Afrika"
"Mimi niko hapa kwa sababu moja tu, kuhakikisha tunafikia malengo hayo, " alisema Gamondi
Yanga inaendelea na pre-season Avic Town ambapo wiki ijayo kikosi kinatarajiwa kuelekea Afrika Kusini kuendelea na program nyingine za pre-season