Abuya amn'goa Skudu Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jul 2024
Abuya amn'goa Skudu Yanga

Jana usiku Yanga ilitambulisha usajili wa winga Duke Abuya aliyetua kutoka klabu ya Singida Black Stars

Abuya ni pendekezo la Kocha Miguel Gamondi akiamini winga huyo raia wa Kenya ataongeza ubora katika safu yake ya ushambuliaji kutokea pembeni

Ujio wa Abuya unamaanisha winga Skudu Makudubela safari yake na Yanga imeishia hapo

Skudu alijiunga na Yanga msimu uliopita akitokea Marumo Gallants. Ushindani wa nafasi katika kikosi cha kwanza ulimfanya asionekane mara kwa mara uwanja

Abuya ni winga wa tofauti kwani licha ya kushambulia, anaweza kuisaidia timu pale inapokuwa haina mpira

Abuya anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Yanga katika dirisha hili baada ya Aboubakar Khomein, Chadrack Boka, Aziz Andambwile, Clatous Chama na Prince Dube

Aidha Yanga tayari imesajili nyota wanne wa kigeni huku ikiwa imetangaza kuachana na Augustine Okrah, Joyce Lomalisa na Joseph Guede akijiunga na Singida BS

Skudu na Gift Fred nao wanaweza kuungana na wachezaji waliopewa mkono wa kwaheri

Bado Yanga haijamtambulisha mshambuliaji Jean Baleke ambaye tayari amekamilisha taratibu zote za kujiunga na Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’