Msimu uliopita haukuisha vyema kwa kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua ambaye majeraha aliyopata Machi 17 katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc yalimfanya akae nje miezi miwili na kukosa mechi muhimu za robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns
Kuonyesha amepania kufanya makubwa msimu huu, Pacome amewasili mapema na anajifua sawasawa katika pre-season ya Yanga iliyoanza tangu Jumatatu
Kwa jinsi kikosi cha Yanga kilivyosukwa msimu huu, ushindani miongoni mwa wachezaji utakuwa mkubwa kwani kila mmoja anataka nafasi katika kikosi cha kwanza




ADVERTISE HERE