Klabu ya Kaizer Chiefs leo imezindua michuano ya Toyota Cup ambapo Yanga imealikwa kushiriki
Mabingwa hao wa Tanzania Bara wataumana na wenyeji wao Kaizer Chiefs katika mchezo utakaopigwa Julai 28 katika uwanja wa Toyota huko Afrika Kusini
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amehudhuria hafla ya uzinduzi wa michuano hiyo iliyofanyika Afrika Kusini jana
Ni rasmi sasa Kocha Nasreddine Nabi anakwenda kuchuana na Kocha Miguel Gamondi katika mechi ya kihistoria
Jana Kaizer Chiefs walimtambulisha Nabi kuwa Kocha wao Mkuu
ADVERTISE HERE