Baada ya utambulisho wa Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka', Yanga haikutambulisha mchezaji mwingine mpya kwa siku tano, ikitoa taarifa za wachezaji walioongeza mikataba ya wengine waliopewa mkono wa kwaheri
Lakini majira ya saa sita usiku wa kuamkia kesho Jumapili, Yanga inakwenda kutambulisha usajili wa pili katika dirisha hili
Yanga imeendelea na utamaduni wake wa kuwatambulisha wachezaji 'usiku mnene' na mara nyingi wachezaji wanaotambulishwa katika muda huo ni 'vifaa'
Misimu miwili iliyopita, Stephane Aziz Ki alivunja rekodi kwa kutambulishwa saa tisa usiku
Akizungumza kwa njia ya simu na Wananchi wa Mbeya mapema leo, Hersi aliwaahidi kuwa itakapofika saa 6 usiku watafurahi...!
ADVERTISE HERE