Tuombeeni dua - Nadir

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Apr 2018
Tuombeeni dua - Nadir
Kikosi cha Yanga leo kinatarajiwa kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Hawassa kuelekea mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho.

Nahodha wa Yanga Nadir Haroub amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri tayari kwa mchezo huo.

Akizungumzia hali ya hewa na mji huo, Nadir amesema licha ya hali ya hewa ya baridi lakini haiwezi kuwa kikwazo kwao kutimiza malengo yao ya kutinga makundi.

"Kusema kweli baridi ipo, hali ya hewa ya huku unaweza kufananisha kama mji wa Arusha, lakini ni hali ya hewa nzuri"

Aidha, kuelekea mchezo huo Nadir amesema watacheza kwa tahadhari kubwa kwani wanafahamu uwezo wa wapinzani wao.

"Bado mechi ni ngumu kwa sababu tunacheza na timu nzuri. Lengo letu ni kuhakikisha tunapata bao la ugenini japo hata sare itatuvusha hatua ya makundi, ushindi ndio matokeo tunayohitaji zaidi."

"Nawaomba Watanzania watuombee dua ili tuweze kufanya vizuri. Sisi tuko hapa kuiwakilisha nchi ya Tanzania."
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’