Yanga kubadili utaratibu wa kutoa 'Thank You'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jul 2024
Yanga kubadili utaratibu wa kutoa 'Thank You'

Klabu ya Yanga haitatangaza majina ya wachezaji wanaoachana nao kupitia mitandao ya kijamii

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema klabu inathamini mchango wa wachezaji hao pamoja na kuwa umefika wakati wa kuachana nao

Kamwe amesema katika utafiti aliofanya kama kiongozi, amebaini taarifa za wachezaji hao zinapowekwa mitandaoni hupokelewa kwa hisia tofauti jambo ambalo linaweza kuathiri maisha yao katika klabu mpya wanazokwenda kuzitumikia

"Safari hii hatutaweka taarifa za wachezaji tunaoachana nao kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa tumebaini taarifa hizo hupokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki"

"Wapo baadhi ya mashabiki wanaandika komenti mbaya ambazo huwavunja moyo wachezaji na pia komenti hizo zinaweza kuwaathiri huko wanakoelekea"

"Tutatoa taarifa zao kwa sababu tunafahamu Wanachama wetu wana haki ya kufahamu walioondoka, lakini tutatumia utaratibu wa kiungwana"

"Taarifa ya kuachana na mchezaji sio taarifa ambayo unahitaji kuitangaza kwa lengo la kunufaika kibiashara," alisema Kamwe

Yanga huenda itatoa taarifa moja kuhusu wachezaji wote ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’