Katika moja ya mahojiano aliyofanya msimu uliopita, kiungo Mganda Khalid Aucho alisema kama kuna mchezaji anatamani kucheza nae katika timu moja basi ni Clatous Chama
Aucho alisema amemfahamu Chama muda mrefu na amekuwa akivutiwa na aina yake ya uchezaji
"Ukiniuliza ni mchezaji gani kwa hapa Tanzania nje ya Yanga nitatamani kucheza nae timu moja, nitamtaja Clatous Chama"
"Kwa vile ambavyo Chama anacheza ndivyo mimi hupenda kufanya, anarahisisha mambo uwanjani. Simpigii debe asajiliwe na Yanga lakini ikitokea amesajiliwa basi nitafurahi kuwa nae katika timu moja," alisema Aucho
Aucho amepachikwa jina la utani 'Dokta' kutokana na aina yake ya uchezaji ambapo hufanya mchezo wa mpira wa miguu kuonekana ni rahisi sana
Mwenyewe amekiri kuwa Chama anaifanya kazi hiyo kwa ubora zaidi na ujio wake Yanga ina maana wote wakianza katika mechi kutakuwa na madokta wawili uwanjani...!