Gamondi ataka pre-season mapema

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Jun 2024
Gamondi ataka pre-season mapema

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ametaka kikosi chake kianze pre-season mapema

Huenda wiki ijayo Yanga ikaondoka nchini kuelekea nje ya nchi ambako kambi hiyo ya maandalizi ya msimu mpya itafanyika

Kwa misimu ya karibuni Yanga imekabiliwa na changamoto ya kukosa muda mrefu wa pre-season iwe kwa ratiba kuchelewa au changamoto za kusafiri

Kutokana na ufinyu wa muda, msimu uliopita Yanga ilifanya pre-season yake Avic Town, ambapo kikosi kilijifua kwa wiki mbili tu kabla ya Tamasha la Wiki ya Mwananchi

Gamondi amesema kalenda ya mashindano ya msimu ujao haitoi nafasi kwao kuendelea kusubiri hivyo amehitaji wachezaji wote wawe wamerejea wiki ijayo

"Tuna ratiba ngumu sana mashindano mengi yamekuwa karibu kulingana na kalenda ambayo nimepatiwa, hapa lazima tuanze kujiandaa haraka ili kila kitu kiwe sawa"

"Kila mchezaji anatakiwa kuwahi ili ratiba iwe kwa pamoja, nadhani viongozi watalifanya hili kwa weledi, kuna faida kubwa kama maandalizi ya mwanzo ya msimu yakafanyika kwa kila mtu kuwa hapa," alisisitiza Gamondi

Uongozi wa Yanga umeahidi kutangaza mipango yote kuhusu pre-season siku ya Jumatatu. Siku ambayo pia watatangaza maboresho ya kikosi cha mabingwa hao wa nchi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’