Kamwe akerwa Yanga kutumika na Mawakala

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jun 2024
Kamwe akerwa Yanga kutumika na Mawakala

Klabu ya Yanga imesema kuwa baadhi ya mawakala wanaitumia klabu hiyo kwa ajili ya kuwapa thamani wachezaji wao na kuwauza kwa dau kubwa

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe, amesema baadhi ya Mawakala wa wachezaji wamekuwa na tabia ya kuwahusisha wachezaji kuwa wanatakiwa na Yanga ili kuzifanya timu zingine zipande dau wakati si kweli kama wanawahitaji

Kamwe alisema vitendo hivyo vilifanyika msimu uliopita na anashangaa msimu huu vimeibuka tena, akiwataka Mawakala kuwauza wachezaji kwa thamani zao halisi na kuacha kuitumia Yanga kwa njia ya kuwapandisha thamani na kupata pesa nyingi za usajili

"Mwaka jana hawa mawakala walitengeneza stori kuwa kuna mchezaji Yanga inamtaka, lakini alipokwenda klabu nyingine ikasemekana eti ameibiwa Uwanja wa Ndege, sisi wala hatukusema kitu," alisema Kamwe

Ingawa hakufafanua, lakini ukirejea moja ya stori za matukio ya msimu uliopita ilisemekana kuwa Simba ilimpora mchezaji raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Fabrice Ngoma, Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, akiwa anakuja kusaini mkataba Klabu ya Yanga

"Kuelekea msimu unaokuja tunaanza kusikia tena habari kama zile, wanasema kuna kiungo tumepokonywa, si kweli ukiona hivyo hatukumhitaji, hivyo ni kazi ya Mawakala kupiganisha ili wapige pesa," alisema Ofisa Habari huyo.

Akizungumzia usajili, Kamwe alisema tayari wameshamaliza kazi iliyobaki ni kuwatangaza tu. Tangu awali, Yanga ilitangaza kuwa haitofanya usajili mkubwa sana kwani bado ina kikosi imara, na ilichofanya ni kuzuia wachezaji wake muhimu kubaki, na kufanya usajili wa wachezaji wachache tu wenye viwango vya hali ya juu kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi

"Malengo tuliyonayo ni makubwa na usajili tulioufanya, watu watalia na kusaga meno," alisema Kamwe

Tetesi zinadai kuwa Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji, Emmanuel Bola Lobota, winga kutoka Singida Black Stars, Agee Basiala, kiungo mshambuliaji kutoka AS Maniema Union na beki wa kushoto, Chadrack Boka kutoka Klabu ya Saint Eloi Lupopo, wote hao kutoka DR Congo

Mwingine ni kipa Khomein Abubakar wa Singida Black Stars, anayekwenda kuchukua nafasi ya Metacha Mnata, anayetajwa kuondoka

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’