Boka ajipanga kuanza maisha Jangwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jun 2024
Boka ajipanga kuanza maisha Jangwani

Ni suala la muda tu, Yanga itamtambulisha mlinzi mpya wa kushoto Chadrack Boka aliyetua kwa Wananchi akitokea klabu ya Fc Lupopo ya DR Congo

Boka ni usajili wa kwanza kukamilishwa na Yanga katika dirisha hili la usajili ambalo limefunguliwa rasmi Juni 15

Nyota huyo anasubiri kusajiliwa kwenye mfumo wa usajili wa FIFA Connect ambapo msemaji wa Yanga Ali Kamwe jana alithibitisha kuwa tayari klabu hiyo imelipa madai yote yaliyokuwa yaamefunguliwa na wachezaji wao wa zamani na hivyo wakati wowote timu itafunguliwa kusajili

Boka tayari amepatiwa program maalum ya mazoezi na Kocha Miguel Gamondi ambayo anapaswa kuikamiilisha kabla ya kujiunga rasmi na Yanga katika pre-season

"Kocha amenipigia, akanikaribisha kwenye timu, ameniambia anataka nikaonyeshe uwezo mkubwa ndani ya Yanga kwa upande wa beki wa kushoto, ameniambia nijiandae kwa ushindani kwani ubora wangu ndio utakaonipa nafasi kwa kuwa wapo wachezaji wazuri pia wanacheza eneo hilo"

"Akaniambia kuna msaidizi wake atanipigia kunipa programu ya mazoezi kipindi hiki ligi imemalizika na nitatakiwa kuifuata sawa sawa na kama sitafuata nitaanza kazi kwa adhabu"

"Nimefurahia sana mazungumzo na kocha yamenifanya nijipange vizuri zaidi kwa kuona kuwa na kwenda kufanya kazi na timu yenye kocha mkubwa anayetaka mafanikio lakini zaidi ameniheshimu kwa kuwasiliana na mimi kwanza," Boka alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’