Klabu ya Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs mwisho wa mwezi wa saba
Kaizer Chiefs wamewaalika Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki katika maandalizi ya msimu mpya
Ikumbukwe mwanzoni mwa msimu uliomalizika Yanga alicheza na Kaizer Chiefs katika kilele Cha wiki ya MWANANCHII na kufanikiwa kushinda mchezo huo
Mechi hiyo imeandaliwa na wadhamini wakuu wa Kaizer Chiefs na imepangwa kufanyika mwezi ujao na Uwanja kwa ajili ya mchezo huo utatangazwa baadae

Aidha ni mchezo ambao utawakutanisha Kocha wa zamani wa Yanga Nasreddine Nabi dhidi ya kocha wa sasa Miguel Gamondi
Nabi anatarajiwa kutangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Kaizer Chiefs baada ya kuhitimisha msimu na FAR Rabat iliyomaliza nafasi ya pili ligi kuu ya Morocco