VAR ni uhakika msimu ujao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jun 2024
VAR ni uhakika msimu ujao

Serikali imependekeza kutoa msamaha wa kodi katika uingizaji mashine za mfumo wa video za kusaidia marefa kutoa uamuzi sahihi uwanjani (VAR)

Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, aliyasema hayo bungeni jana alipowasilisha mapendekezo ya Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2024/25, akisisitiza kuwa VAR itaondoa malalamiko ya timu kupendelewa na marefa

"Msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara tutaanza kutumia "VAR" ili kuhakikisha matokeo yanayopatikana uwanjani yanakuwa ya haki maana kuna timu zimezidi - msimu mmoja penati 10, halafu zikifungwa zenyewe magoli yanakataliwa"

"Na ili tuwe na ''VAR'' za kutosha katika viwanja vyote, ninaleta pendekezo la kutoa msamaha kwenye uingizaji mashine za ''VAR'' na vifaa vyake kwa ufafanuzi utakaotolewa hapo baadaye. Inawezekana!" Dk. Mwigulu alisisitiza

Waziri huyo pia alisema serikali inatambua umuhimu wa michezo, sanaa na burudani katika kukuza ajira hususani kwa vijana. Kwa kuzingatia hilo, imeendelea kuunganisha wasanii wa Tanzania na soko la kimataifa kupitia mikutano na matamasha mbalimbali na kuhakikisha kuwa kazi za ubunifu wao zinalindwa

Alisema serikali imeendelea kujenga misingi ya uibuaji na uendelezaji vipaji kuanzia shuleni ambayo imesaidia kuongeza ajira na kipato kwa wachezaji wanaosajiliwa katika timu mbalimbali ndani na nje ya nchi

"Kufuatia hatua hiyo ya uendelezaji vipaji, imewezesha timu ya taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars) kushiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mara ya tatu katika historia ya taifa letu na Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kufuzu kucheza mashindano ya WAFCON ambayo yatafanyika mwaka 2024 Morocco

"Kufuatia jitihada za makusudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha sekta ya michezo nchini, Tanzania itakuwa mwenyeji wa michuano ya AFCON mwaka 2027 kwa kushirikiana na nchi za Uganda na Kenya"

"Nipende kuwahakikishia kuwa serikali imejipanga vyema juu ya maandalizi ya michuano hiyo ikiwamo ujenzi wa Uwanja wa Samia jijini Arusha kama alivyowasilisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo," alisema

Alitoa rai kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuanza maandalizi ya Taifa Stars mapema ili hatimaye kombe hilo libaki nyumbani

"Maandalizi ya timu yanahitaji kuwapo viwanja bora. Serikali imejiandaa kujenga viwanja vipya na kukarabati baadhi ya viwanja vilivyopo. Kuhusu ubora wa kiwanja (pitch) kwenye viwanja mbalimbali, tayari serikali ilitunga sheria inayotoa msamaha kwenye uingizaji nyasi bandia na vifaa vyake," alisema

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’