Ukizungumzia mafanikio makubwa ambayo Yanga Princess imewahi kupata katika ligi kuu ya Wanawake ni msimu wa 2021/22 ambapo kinadada hao walimaliza nafasi ya pili wakitofautiana alama moja tu na Simba Queens iliyotwaa ubingwa. Wakati huo Yanga Princess ilikuwa ikinolewa na Edna Lema 'Mourinho'
Baada ya msimu huo Yanga iliachana na Edna ambaye yuko mbioni kukamilisha mafunzo yake ya ukocha Diploma A ya CAF
Edna akatua klabu ya Biashara United ya Mara akiwa Kocha Msaidizi na pengine anakaribia kuandika rekodi ya kushiriki kuirejesha Biashara United ligi kuu
Jana Biashara United walishinda mechi ya kwanza ya play-off dhidi ya Tabora United na wana dakika nyingine 90 za kulinda ushindi wao wa bao 1-0 ili kuhakikisha wanarejea Ligi Kuu
Licha ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na uongozi wa Yanga kwa Yanga Princess, tangu kuondoka kwa Edna unaweza kusema Yanga Princess imepoteza mwelekeo licha ya kunolewa na kocha wa kigeni kutoka Zambia
Mkataba wa Edna na Biashara United unamalizika mwezi huu na tayari Yanga imeanza mchakato wa kumrejesha kuinoa Yanga Princess
Kuna uwezekano mkubwa msimu ujao Edna ndiye atakayekuwa Kocha wa Yanga Princess