Djuma Shabani kutoka Yanga hadi Coastal Union

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jun 2024
Djuma Shabani kutoka Yanga hadi Coastal Union

Klabu ya Coastal Union imekamilisha usajili wa mlinzi wa zamani wa Yanga Djuma Shabani 'Soldier ya Bemba'

Djuma anajiunga na Coastal Union akiwa mchezaji huru baada ya kukaa msimu mzima pasipo kuwa na timu

Baada ya misimu miwili ya mafanikio na Yanga, Djuma na Yannick Bangala 'wakatikisa kiberiti' kwa uongozi wa Yanga wakitaka kuvunja mikataba yao

Baada ya mvutano wa ndani kwa ndani, hatimaye uongozi wa Yanga ukaridhia wachezaji hao kuondoka lakini kwa kufuata utaratibu

Azam Fc ambao walikuwa wakiwashawishi nyuma ya pazia, wakajitokeza hadharani na kuwanunua wachezaji wote wawili Yanga ikipokea kitita cha Tsh Milioni 200

Yanga iliridhia wachezaji hao kuondoka baada ya ripoti ya Nasreddine Nabi, aliyekuwa mkufunzi wa Yanga wakati huo kupendekeza kwa uongozi kuachana nao

Bahati mbaya kwa Djuma akashindwa kuitumikia Azam Fc baada ya dirisha la usajili kufungwa kabla ya mchakato wake wa usajili kukamilika

Azam Fc walimuahidi watamuongeza katika usajili wa dirish dogo hivyo akaendelea kujifua na timu hiyo

Hata hivyo dirisha dogo lilipofungulia Azam FC wakamgeuka baada ya kocha wao kutoridhishwa na kiwango chake

Djuma ni kama anakwenda kuanza upya Coastal Union, bila shaka kuna somo amejifunza..!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’