Baada ya kuhitimisha msimu kwa kubeba taji la Shirikisho la CRDB, wachezaji wa Yanga wamepewa mapumziko ya mwezi mmoja
Mabingwa hao wa kihistoria ligi kuu ya Tanzania Bara watarejea tena Avic Town mwanzoni mwa Julai 2024 kwa ajli ya kuanza maandalizi ya msimu mpya 2024/25
Aidha kwa wachezaji wenye majukumu ya timu za Taifa wao wameelekea kujiunga na timu zao kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu kombe la Dunia
Wachezaji wa Yanga walioitwa timu za Taifa ni Aboutwalib Mshery, Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto, Mudathir Yahya na Clement Mzize
Wengine ni Djigui Diarra, Khalid Aucho, Stephane Aziz Ki na Kennedy Musonda
Mwezi Julai Yanga inatarajiwa kushiriki michuano ya Kagame Cup inayotarajiwa kuanza Julai 19 jijini Dar es salaam
ADVERTISE HERE