Tutaboresha ili tuwe bora zaidi - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jun 2024
Tutaboresha ili tuwe bora zaidi - Kamwe

Baada ya kufanikiwa kutetea mataji mawili ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la CRDB,  Yanga imepania kufanya maboresho zaidi ili kuhakikisha inaendeleza ubabe katika soka la ndani na kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao

Kwa msimu wa tatu mfululizo, Yanga ni bingwa wa ligi kuu na itaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Msimu uliomalizika, Yanga ilitolewa katika mashindano hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwenye hatua ya robo fainali

Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ally Kamwe, amesema kutakuwa na maboresho muhimu katika kila idara ili wafanye vizuri katika mashindano yote watakayoshiriki 2024/25

Kamwe alisema wanafahamu mashindano hayo ya ngazi ya vilabu Afrika ni magumu, hivyo hawataki 'kuishia' tena njiani na wanataka kuipa heshima Tanzania

"Kila msimu tunakuwa na malengo yetu, tunapanga vizuri kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, tunataka kufanya vizuri zaidi, tunataka kuonyesha hatukufanya vizuri msimu uliopita kwa bahati mbaya"

"Mchezaji ambaye Yanga tunamhitaji hatutamwacha, lakini tutaboresha kikosi chetu kwa mapendekezo ya kocha wetu, tunataka kuwa na Yanga tishio zaidi ya hii, Wana-Yanga watafurahi msimu ujao," alisema Kamwe

Baada ya msimu kufika tamati, wachezaji wanatarajiwa kupewa mapumziko ya mwezi mzima wakitarajiwa kurejea mwanzoni mwa mezi Julai tayari kuanza maandalizi ya 2024/25

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’