Leo majira ya saa 2 mpaka saa 4 usiku macho na masikio ya Wananchi yataelekezwa visiwani Zanzibar katika mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la CRDB ambapo miamba miwili ya soka Tanzania Bara Yanga na Azam Fc itaumana
Yanga na Azam Fc zinajenga upinzani unaozidi kukua ambapon msimu huu Azam Fc wamechukua nafasi ya Simba wakiwa wapinzani wa kweli wa Wananchi
Itakuwa mechi bora ya kuhitimisha msimu wa mashindano na bila shaka Wananchi wa Zanzibar watashuhudia burudani ya aina yake katika uwanja wa New Amaan Complex kuanzia saa 2:15 usiku
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo baada ya kuwa na muda wa kutosha wa maandalizi
Gamondi alionekana kuvutiwa na ubora wa 'pitch' ya New Amaan Complex na kuwahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa wanakwenda kuishuhuhdia timu yao ikiwa kwenye ubora mkubwa
Hata hivyo Gamondi alisisitiza kuwa hawaendi katika mchezo huo wakiwa na fikra za kulipa kisasi, ni lazima wawaheshimu wapinzani wao kwani anaamini wana timu nzuri
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana kwenye ligi uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 katika mchezo ambao wachezaji Yao Kouassi na Pacome Zouzoua walipata majeraha ambayo yaliwaweka nje kwa muda mrefu
Habari njema kwa Wananchi ni kuwa nyota hao wako fit na huenda wakawa sehemu ya kikosi leo
Yanga inasaka taji la FA kwa msimu wa tatu mfululizo, wakitoka kushinda taji hilo msimu uliopita kwa kuifunga Azam Fc bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa Mkwawani