Baada ya taarifa za Yanga kuachana na kipa Metacha Mnata, timu ya Ihefu inatajwa kuwa katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wake
Metacha aliwahi kuichezea Singida Big Stars kabla ya kubadilishwa na kuwa Singida Fountain Gate akitokea Yanga, kabla ya kurejea tena Jangwani
Mmoja wa viongozi wa Ihefu, amethibitisha kuwa katika mchakato wa kumsajili mlinda lango huyo ambapo amesema kwamba mazungumzo yamefikia pazuri
"Metacha ni kipa mzuri na tumefuatilia tumeona Yanga hawatakuwa na mpango wa kuendelea naye ndio maana tumeweka nguvu ya kuhitaji huduma yake," alisema kiongozi huyo
Metacha amekuwa nje ya kikosi cha Yanga ikielezwa alisimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu
Yanga inatarajiwa kusajili mlinda lango mwingine wa wa ndani kuchukua nafasi yake