Jumamosi May 25 2024 mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga watakabidhiwa kombe la Ligi Kuu ya NBC 2023/24 baada ya kufanikiwa kulitetea kwa msimu wa tatu mfululizo
Katika kufanya siku hiyo kuwa ya kipekee, NBC Bank ambao ni Wadhamini wa Ligi, wameandaa matukio ya aina yake jijini Dar es salaam
Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya UMMA Bank ya NBC Godwin Semunyu amesema NBC Bank imeboresha soka la Tanzania kwa kutoka zaidi ya bilion 32.6 uwekezaji ambao haukuwahi kufanyika kabla. Aidha NBC Bank inashirikiana na Yanga kwenye utoaji wa kadi za wanachama na mashabiki
"Sisi kama Benki ya NBC tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunaboresha soka la Tanzania kwa kutoka zaidi ya bilion 32.6 jambo ambalo halijawahi kufanyika. Tumeboresha kwenye baadhi ya maslahi ya Wachezaji"
"Tumeamua kushirikiana na Yanga kwenye utoaji wa kadi za wanachama ambazo zinasaidia kwenye mambo mbalimbali. Kwanza kadi hizi zimeunganishwa na VISA, N-card ambapo unaweza kununua tiketi za uwanjani. Kadi hizi zinapatikana kwenye matawi yetu yote," alisema Semunyu
Akizungumza katika Mkutano huo wa pamoja na Wanahabari kati ya Yanga na NBC Bank, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema Helkopta (chopa) maalum imeandaliwa kwa ajili ya kufanya paredi la ubingwa jijini Dar es salaam
"Kuanzia saa 5 asubuhi kutakuwa na Helkopta itakayofanya paredi ya ubingwaΒ ndani ya Jiji la Dar es salaam"
"Hili litakuwa tukio la kwanza na la aina yake kufanyika hapa Afrika, sisi tunakwenda kuwafundisha namna ubingwa unasherehekewa"Β
"Baada ya kufanya parade maeneo mbalimbali, saa 9 Alasiri Helkopta itatua uwanja wa Benjamin Mkapa kuleta kombe"
"Yaani wakati mashabiki wa Yanga wakiwa tayari wameujaza uwanja wa Mkapa, Helkopta itatua, kombe litakabidhiwa kisha itaondoka," alisema Kamwe
Yanga ni mabingwa tangu Bank ya NBC ilipoanza kudhamini ligi kuu ya Tanzania Bara
Likiwa taji la tatu ambalo Yanga watakabidhiwa kuwa mali yao, NBC Bank wameamua kuifanyia Yanga sherehe kutokana na mafanikio hayo