Matchday : Yanga vs Ihefu Fc, FA Cup SF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 May 2024
Matchday : Yanga vs Ihefu Fc, FA Cup SF

Baada ya Azam Fc kutangulia fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union, mechi ya pili ya nusu fainali kati ya Yanga dhidi ya Ihefu Fc inapigwa leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha

Wakiwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo kwa misimu miwili mfululizo, Yanga inasaka rekodi ya kutinga fainali ya tatu mfululizo na pengine kubeba taji kwa mara ya nne tangu kuanzishwa kwake

Hata hivyo Wananchi leo wanakabiliwa na timu ngumu ya Ihefu Fc ambayo mara nyingi sio wepesi wanapocheza na Yanga licha ya kubugizwa mabao 5-0 mara ya mwisho timu hizo zilipokutana katika ligi kuu ya NBC

Yanga tayari ni mabingwa wa ligi kuu hivyo nguvu zote zimeelekezwa katika kuhakikisha wanabeba na taji la FA

Kitendo cha Azam Fc kutinga fainali hapo jana ni kama kimewaongezea 'mzuka' Wananchi kuhakikisha wanashinda leo dhidi ya Ihefu Fc na kukutana tena na Azam Fc katika fainali kama msimu uliopita

Wananchi wana deni na Azam Fc wakikumbuka kipigo cha mabao 2-1 mara ya mwisho timu hizo zilipokutana kwenye ligi

Mchezo utapigwa saa 9:30 Alasiri...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
1h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
13h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
22h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’