Ni katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la CRDB kati ya Yanga dhidi ya Ihefu Fc utapigwa hapo kesho. Yanga iko tayari kusaka fainali ya tatu mfululizo katika michuano hiyo
Azam Fc tayari wametangulia fainali baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba leo
Kama Yanga itafanikiwa kutinga fainali, basi fainali ya msimu huu itakuwa marudio ya msimu uliopita ambapo Yanga na Azam Fc zilichuana katika mchezo uliopigwa hapo hapo Sheikh Amri Abeid Yanga ikiibuka mabingwa kwa ushindi wa bao 1-0
Ni kesho saa 9:30 Alasiri katika uwanja uleule ambao Yanga ilibeba ubingwa msimu uliopita...





ADVERTISE HERE