Yanga yasitisha sherehe za ubingwa kwa muda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 May 2024
Yanga yasitisha sherehe za ubingwa kwa muda

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wamesitisha shamrashamra za ubingwa wa ligi kuu ya NBC kwa muda ili wajikite kwenye maandalizi ya mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Ihefu Fc utakaopigwa Jumapili, May 19 mkoani Arusha

Kamwe amewataka Wanachama na Mashabiki wa Yanga kuweka nguvu zao katika mechi hiyo ili kuhakikisha wanakata tiketi ya kutinga fainali

Kuhusu shamrashamra za ubingwa, Kamwe amesema watatangaza baada ya kumalizana na Ihefu Fc

"Kwa sasa tumesitisha shamrashamra za ubingwa wa 30 wa ligi kuu kwa muda, mbele yetu tunakabiliwa na mechi ngumu ya nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Ihefu Fc"

"Ihefu Fc ni miongoni mwa timu chache ambazo tumegawana nazo pointi msimu huu. Walitufunga mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa ligi na sisi kuwafunga mabao 5-0 katika mchezo wa pili"

"Tunakutana nao tena katika nusu fainali ya FA, tunafahamu haitakuwa mechi nyepesi, tayari timu iko kambini kujiandaa na mchezo huu"

"Niwaombe wapenzi, wanachama na mashabiki wetu kuwa tunapaswa kuungana na kuipa sapoti timu yetu ili kuhakikisha tunapata ushindi"

"Najua wengi wana shauku ya kufahamu kuhusu parade la ubingwa wa ligi kuu, niwaambie tu, kwa sasa tumalizane kwanza na Ihefu Fc, baada ya hapo tutatangaza kila kitu," alisema Kamwe

Yanga imepania kutetea taji la FA kwa msimu wa tatu mfululizo kama walivyofanya katika ligi kuu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’