Mzize awania ufungaji bora kombe la FA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 May 2024
Mzize awania ufungaji bora kombe la FA

Mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize ndiye kinara wa ufungaji katika michuano ya kombe la Shirikisho la CRDB Bank

Akiwa amecheza mechi zote nne za Yanga kuanzia hatua ya awali, Mzize amepachika mabao matano

Kuelekea mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ihefu Fc utakaopigwa Jumapili, May 19 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha, Kocha wa Yanga Miguel Gamondi huenda akaendelea kumuamini Mzize kuongoza safu yake ya ushambuliaji katika michuano hiyo

Pengine itakuwa nafasi kwake kuzidi kujiwekaa katika nafasi ya kuibuka mfungaji bora katika michuano hiyo

Msimu huu Yanga huenda ikatawala katika tuzo kwenye kila eneo kwani imefanya vizuri katika kila eneo

Kwenye Ligi Kuu ya NBC Stephane Aziz Ki anawania ufungaji bora akichuana na Feisal Salum wote wakifunga mabao 15

Aziz Ki pia anaongoza kwenye assist akiwa nazo nane sawa na Kipre Junior wa Azam Fc

Mlinda lango Djigui Diarra anachuana na Vumi Ley Matampi wa Coastal Union katika kuwania tuzo ya kipa bora wote wakiwa na 'cleensheet' 13

Ukizungumzia kocha bora jina ni moja, Miguel Gamondi ambaye ameiongoza Yanga kutwaa ubingwa ligi kuu huku ikiwa na mechi tatu mkononi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
3h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’